John 6:15-21

15 aYesu akijua kwamba walitaka kuja kumfanya awe mfalme wao, kwa nguvu, akajitenga nao akaenda milimani peke yake.

Yesu Atembea Juu Ya Maji

(Mathayo 14:22-33; Marko 6:45-52)

16 bIlipofika jioni, wanafunzi wake waliteremka kwenda baharini. 17Wakaingia kwenye mashua, wakaanza kuvuka bahari kwenda Kapernaumu. Wakati huu kulikuwa tayari giza na Yesu alikuwa hajajumuika nao. 18Bahari ikachafuka kwa sababu upepo mkali ulikuwa unavuma. 19 cWanafunzi walipokuwa wamekwenda mwendo wa karibu maili tatu au nne,
Maili tatu au nne ni kama kilomita 5 au 6.
walimwona Yesu akitembea juu ya maji akikaribia mashua, nao wakaogopa sana.
20 eLakini Yesu akawaambia, “Ni mimi. Msiogope.” 21Ndipo wakamkaribisha kwa furaha ndani ya mashua, na mara wakafika ufuoni walikokuwa wakienda.

Copyright information for SwhNEN